Leo Jumamosi, Januari 31, 2026, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (Certificate of Secondary Education Examination – CSEE) 2025.
Taarifa hii imethibitishwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania.
Katika matokeo hayo:
Ufaulu wa kitaifa umeongezeka na kufikia asilimia 94.98%, ikionyesha ongezeko la takriban 2.61% ikilinganishwa na mwaka wa 2024
Wanafunzi waliofaulu kwa kupata madaraja ya Division I, II, III na IV ni 526,620.
Idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani ilikuwa kubwa, na jumla ya 569,883 wanafunzi wa shule na 25,927 wanafunzi binafsi.
Matokeo haya ni muhimu kwa wanafunzi wanaotarajia kuendelea na kidato cha tano, vyuo vya ufundi, au mwelekeo mwingine wa taaluma.
Taarifa Muhimu Zaidi kuhusu matokeo ya kidato CHA nne.
Aidha, vyombo vya habari pia vimereport kuwa baadhi ya matokeo yamefutwa kwa wanafunzi 77 kutokana na ukwepaji wa taratibu za mtihani.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato cha Nne 2025 (NECTA)
Unapo taka kuona matokeo yako binafsi, fuata hatua hizi rasmi:
Kupitia Mtandao (Online)
1.Tembelea tovuti rasmi ya NECTA:🔗https://www.necta.go.tz/
2.Nenda kwenye sehemu ya “Matokeo” au “Results”.
3.Chagua CSEE (Kidato cha Nne).Chagua mwaka 2025/2026.
4.Ingiza namba yako ya mtihani (Index Number) na/au jina la shule.
5.Bonyeza Angalia Matokeo kuona alama zako
Hapa ni baadhi ya link zinazofanya kazi kwa kuangalia matokeo mara moja (zinaweza kubadilika kadri tovuti inavyosasishwa):
https://onlinesys.necta.go.tz/
Kupitia SMS
. Tumia muundo:NECTA <space> CSEE <space> INDEX_NUMBER
. Tuma SMS kwenda namba husika ya huduma (hutoa taarifa ya matokeo kupitia ujumbe mfupi).
Vidokezo Muhimu kwa Wanafunzi na Wazazi
. Hakikisha una namba sahihi ya mtihani kabla ya kujaribu kuangalia matokeo.
. Tovuti rasmi ya NECTA inaweza kuwa na msongamano baada ya kutangazwa kwa matokeo; jaribu tena ikiwa hauwezi kuingia mara ya kwanza.
. Endapo kutakuwa na matatizo ya kiufundi au matokeo hayapo, wasiliana na shule yako au ofisi ya NECTA kwa msaada.
Soma hii pia:https://tanzanianews.top/team-usa-mens-hockey-olympic-roster-breakout-players-to-watch/
Hitimisho
Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 yanayotolewa leo yanadhihirisha maendeleo mazuri ya kitaaluma kwa wanafunzi Tanzania.
Ufaulu uliongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita, na sasa wanafunzi wengi wanaweza kuchukua hatua kwa ajili ya masomo ya juu au fursa zingine za taaluma.