Breaking news

Ukraine yafanya mashambulizi makubwa huko Bryansk Kwa kutumia drons

Ukraine imefanya mashambulizi ya droni na kulilenga eneo la Urusi la Bryansk na hivyo kusababisha kukatika kwa umeme, huku mamlaka zikiyataja mashambulizi hayo kuwa miongoni mwa makubwa zaidi tangu kuanza kwa vita hivyo.

Gavana wa Bryansk Alexander Bogomaz amesema mashambulizi hayo yaliyodumu kwa zaidi ya saa 12 na yaliyolenga miundombinu ya nishati yameziacha manispaa tano na sehemu kadhaa za jiji hilo bila umeme wala uwezo wa kupasha joto majumba

Urusi ambayo imekuwa mara kwa mara ikilenga miundombinu ya nishati ya Ukraine, imesema imefanikiwa kudungua droni 170 huko Bryansk, mji unaopakana na Ukraine ambayo pia ilishambulia bandari ya Urusi ya Taman katika Bahari Nyeusi na kuwajeruhi watu wawili.

Bryansk ni mji wa kimkakati unaopakana na Ukraine,jambo linaloufanya kuwa katika hatari ya mara kwa mara wakati wa mapigano.

wakati huo huo ,Urusi imekuwa ikishutumu Ukraine kwa kulenga miundombinu ya kiraia,huku nayo ikiendelea kushambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine kama sehemu ya mkakati wa kivita.

Vita kati ya Urusi na Ukraine vinaendelea kuathiri maisha ya maelfu ya watu katika pande zote mbili.Mashambulizi haya ya karibuni yanainyeaha jinsi vita hiyo inayoendelea kupanuka na kuathiri hata maeneo ya ndani ya Urusi.

Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaonya kuwa mashambukizi ya kulipizana yanaweza kuongeza hatari ya kuongezeka Kwa mzozo huo.

Kwa sasa, mamlaka za Urusi zinaendelea kurekebisha miundombinu iliyoathirika huku zikichunguza atharu kamili za mashambukizi hayo.

Dunia inaendelea kufatilia Kwa karibu maendeleo ya vita hivi vinavyoendelea kubadili taswira ya usalama wa kieneo na kimataifa.

Mwisho

Zaidi ya hayo, tukio hili limezua mjadala mpana kuhusu usalama wa miundombinu muhimu wakati wa vita,hasa katika maeneo ya mpakani kama Bryansk,Wataalamu wa masuala ya ulinzi wanaeleza kuwa matumizi ya droni yamebadilisha sura ya vita vya kisasa Kwa kuwa hurusu mashambulizi ya mbali yenye gharama nafuu lakini athari kubwa.

Hali hii inaongeza shinikizo Kwa pande zote mbili kuimarisha mifumo yao ya ulinzi wa anga na kulinda huduma za msingi kama umeme.maji na nishati.ambazo zinaathiri Moja Kwa Moja maisha ya raia.

Soma habari YOTE:https://www.operanewsapp.com/tz/sw/share/detail?news_id=4c790addb9fce640c23fcb4ff86a8436&news_entry_id=s45afd632260216sw_tz&open_type=tanscoded&request_id=news_19862f1e-6581-4412-baf8-539cb229f683&from=news

Soma hii pia:https://tanzanianews.top/2026/02/15/skoltech-university-scholarship-2026-russia/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *